Thursday, 19 May 2016

NEC imeikabidhi NIDA mashine za utambuzi BVR.


Tume ya taifa ya uchaguzi imewakabidhi mamlaka ya vitambulisho vya taifa,NIDA,mashine za utambuzi zijulikanazo kama
BIOMETRIC VOTER REGISTER,BVR,ili ziweze kuwasaidia kukamilisha kazi ya kuandikisha wananchi ambao bado hawajaandikishwa kutokana na uhaba wa vifaa hivyo hususan maeneo ya vijijini.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa mashine hizo, meneja wa mifumo na uchambuzi,JUMANNE MASHAKA,ambae alimwakilisha mkurugenzi mkuu wa NIDA,amesema mashine hizo zitasaidia kurahishisha kazi ya uandikishaji  kutokana na awali kuwa na mashine 1505 na sasa wamepata mashine 5000.

Kuhusu tofauti ya uwezo wa mashine walizokuwa nazo mamlaka hiyo na za sasa ,meneja huyo amesema watawaachia wataalamu wa IT waaangalie uwezekano wa kuziongezea uwezo mashine hizo ili zikidhi viwango vya NIDA.

Kwa upande wake AMOS MADAHA kaimu mkuu idara ya daftari la kudumu la wapiga kura-TUME ya Taifa ya Uchaguzi amesema wao wanatekeleza agizo la serikali lililowataka kukabidhi mashine hizo NIDA, ili kupunguza gharama za kuagiza zingine na pia kuwarahishia kazi wenzao ili waweze kutimiza jukumu la kuwasajili wananchi.

No comments:

Post a Comment