Saturday 14 May 2016

Wakazi wa jiji la mwanza waandamana kisa kikiwa hivi.

 
Baada ya wanawake sita kubakwa na makundi ya watu wasiofahamika katika pori la makaburi ya kata ya Igoma wilayani Nyamagana Jijini Mwanza, mamia ya wakazi wa kata hiyo leo wameungana kulaani unyama huo, huku wakilitaka Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza kuimarisha doria katika eneo hilo.

Katika eneo hili ambalo pia majambazi na vibaka hulitumia kama kichaka cha kujificha baada ya kufanya uhalifu, wakazi hao wakiongozwa na wenyeviti wa mitaa minne ya Mtakuja, Mkapa, Kilimo “B” pamoja na Shamaliwa “B” wamelifyeka pori hilo, zoezi lililokwenda sambamba na kufanya usafi wa makaburi.

Kutokana na tatizo hilo viongozi wa mitaa hiyo wamepiga marufuku shughuli za ujenzi zinazofanywa na baadhi ya watu, waliovamia maeneo ya Makaburi kuendesha shughuli za kibiashara kama vile ufyatuaji wa matofali, kwa kuwa kufanya hivyo kunachangia kulibana eneo hilo, hatua inayosababisha baadhi ya watu kukosa mahala pa kuzika ndugu zao.

Kwa kuwa uhalifu ni moja kati ya matukio yanayoisumbua kata ya Igoma, viongozi wa mtaa wa mtakuja, Shamaliwa “B”, Kilimo “B” pamoja na mtaa wa Mkapa, wameamua kupitisha azimio la pamoja la kujilinda wao wenyewe, ili kunusuru usalama wa maisha yao na mali zao kutokana na matukio ya uvamizi wa mara kwa mara

No comments:

Post a Comment