Tuesday 3 May 2016

Baraza la Madiwani la mkataa afisa Elimu

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera, limemkataa Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya hiyo, Hellen Lugumila, kwa tuhuma za uzembe na kusababisha wilaya hiyo kuwa ya mwisho katika matokeo ya shule za sekondari kimkoa.

Baraza hilo pia limesema limechukua hatua hiyo kwa kusema kuwa Afisa Elimu huyo ameshindwa kusimamia ipasavyo walimu walioshindwa kuwajibika katika kusimamia elimu mkoani humo ambao wapo chini yake.

Baraza hilo limemtaka Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, kumpangia kituo kingine cha kazi afisa elimu huyo tofauti na wilaya ya Misenyi, na kusema ufanyike mchakato wa haraka wa kupata afisa elimu mwingine kwa sekondari katika wilaya hiyo.

Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo alitoa ushauri wakati wa kikao hicho cha baraza la madiwani katika halmashauri hilo kuhusu kuondolewa kwa afisa huyo jambo ambalo liliungwa mkono na mwenyekiti Adeodatus Rugaibula, diwani wa kata ya Bukwali. na hatimaye wakafikia hatua ya kupiga kura kumuondoa Afisa elimu huyo.

No comments:

Post a Comment