Tuesday 3 May 2016

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya atoa siku 7 kwa Mkurugenzi Hospitali ya Rufaa mbeya kuhusu mjamzito kupingwa kofi.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amos Makala ametoa muda wa siku 7 kwa Mkurugenzi Hospitali ya Rufaa Mbeya, Dk. Goodlove Mbwanji, kufanya uchunguzi na kutoa ripoti kuhusu muuguzi kumpiga mama aliyekuwa akijifungua.
Bwn. Makala ameyasema hayo alipofanya ziara ya kushitukiza katika hospitali hiyo kitengo cha wazazi Meta na kupata malalamiko kutoka kwa mwanamke mmoja kwamba alinyanyaswa na kupigwa kofi la uso wakati akijifungua.

''Mimi nilikuwa nasukuma mtoto nesi akanipiga kofi la uso na mtoto alipofanikiwa kutoka akamkata kitovu amamchukua akanirushia kifuani haya chukua litoto lako ulilokuwa unataka, nikamuuliza nesi mbona kama mwanangu ni mzima amechoka tuu''- Amesema Salome Waya ambaye ndiye amedai kutendewa hivyo.

Kufuatia hali hiyo Makala akakasirishwa na tukio hilo na na kusema kwamba serikali inachukiwa na watu wachache kutokana na uzembe wa watu wachache na kufanya upekuzi wa faili la mama huyo ili kumbaini muuguzi huyo ndipo ikabainika kuwa Bi. Beatrice Sanga ndiye alimhudumia mama huyo April 29 2016.

Mtoto huyo kwa sasa anaendelea vizuri katika chumba cha watoto wanaopewa joto ili aweze kuwa salama na baadaye kukabidhiwa mama yake.

Aidha Mkurugenzi wa hospitali hiyo amesema kwamba atafanya kazi aliyopewa na kufanya maamuzi na atatoa ripoti hiyo kwa mkuu wa wa mkoa kwa muda aliopewa.

No comments:

Post a Comment