Lowassa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kata ya Moita Bwawani ambapo pamoja na mambo mengine amewashukuru wananchi waliompigia kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
''Wanakuja Simanjiro, Kiteto, Ngorongoro, Longido hawatuwezi na wakitaka waje maeneo haya walinganishe na maeneo yao hawatuwezi, ninawashukuru sana kwa kuhama na mimi toka CCM kwenda Chadema''
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Salum Mwalimu amesema chama chao siyo chama cha upembuzi yakinifu na urasimu bali chama chao ni chama cha kufanya kazi kwa vitendo ambapo watahakikisha wanapeleka maji eneo la Moita Bwawani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Isack Joseph amewataka watendaji na wenyeviti wa vijiji kutokuruhusu wakandarasi kufanya kazi bila wao kupata barua na kujirishisha na miradi itakayotekelezwa na kuhakikisha wanaisimamia ili iwe na tija kwa wananchi
No comments:
Post a Comment