Waziri Lukuvi amemgonganisha Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga na mtangulizi wake Edward Lowassa, kuhusu shamba la Makuyuni lililopo jimboni humo.
Lukuvi alifanya hivyo wakati akitoa majibu ya hoja mbalimbali za wabunge kuhusu hotuba ya bajeti yake, lakini Kalanga katika mchango wake alilalamikia kuchelewa kwa utekelezaji wa uamuzi wa Serikali wa kurejesha mashamba makubwa kwa wananchi, likiwamo la Makuyuni.
Akijibu hoja hilo, Lukuvi alimwambia Kalanga kuwa shamba hilo la Makuyuni litarudishwa kwa wananchi, lakini itakula kwake kwa kuwa liko kwa Lowassa.
“Rais Mkapa (Benjamin) aliamua shamba hilo lirudi kwa wananchi na Lowassa ndiye aliyesaini hati ya shamba hilo,” alisema Lukuvi.
Alisema kuwa atahitaji ushirikiano wa Kalanga na halmashauri ya Monduli, kulikabidhi shamba hilo kwa wananchi.
Wakati huo huo, Lukuvi amepiga marufuku watu wote wenye mashamba makubwa ambao wanayapima na kuuza viwanja, waache kwa kuwa haliruhusiwi kuanzia sasa.
“Kama ni shamba litabaki kuwa shamba kama mtu alinunua shamba anataka kubadilisha liwe kiwanja imekula kwake,” alisema Lukuvi na kuongeza kama kuna mtu anataka kufanya hivyo akabidhi shamba kwa halmashauri ili ligawiwe au kuuzwa
No comments:
Post a Comment