Monday, 23 May 2016

Haya ndio maamuzi ya mahakama ya kisutu kuhusu Kesi ya Wachina ya kusafirisha nje meno ya tembo.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuwasomea maelezo ya awali ya shitaka washtakiwa watatu akiwemo raia wa China,Yang Glan wanaokabiliwa na kesi ya kusafirisha nje ya nchi meno ya tembo yenye thamani ya sh.bilioni 5.4 kwa kuwa jalada la kesi hiyo lipo kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).

Kesi hiyo imetajwa  kwa ajili ya washitakiwa hao kusomewa maelezo ya awali mara baada ya upelelezi katika shitaka lao kukamilika.

Wakili wa serikali Shadraka Kimaro aliiambia mahakama kuwa upelelezi katika kesi hiyo umekamilika lakini hawawezi kuwasomea washitakiwa maelezo ya kosa kwa kuwa jalada la kesi hiyo bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Dpp.

Wakili Msemo aliwataja watuhumiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo kuwa ni wafanyabiashara Silivius Matembo na Philimon Manase ambao wanadaiwa kujihusisha biashara ya nyara za serikali,uhujumu  uchumi na kutoroka chini ya ulinzi halali wa askari.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Januari mosi mwaka 2000 na Mei 22 2014 jijini Dar es Salaam.

Ilidaiwa kuwa washitakiwa hao kwa pamoja walijihusisha kuendesha vipande 706 vya meno ya tembo yenye thamani ya sh.5,435,865,000.

Hata hivyo Wakili wa upande wa utetezi Nehemia Nkopo  aliimbaia mahakama kuwa kesi hiyo imekuwa ni ya muda mrefu ambapo ni mara ya nne  imekuwa ikitajwa bila kuendelea chochote mbali na kwamba upande wa mashitaka umeiambia mahakama kuwa upelelezi umekamilika.

Kesi hiyo itakuja June 6 kwa ajili ya washitakiwa kusomwa maelezo ya awali ya kosa lao na watuhumiwa wamerudishwa rumande

No comments:

Post a Comment