Monday, 23 May 2016

Hii ndio changamoto nyingine ya mabasi yaendayo haraka jijin Dar es salaam.

Wiki moja baada ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini dar es salaam kuanza mashine za kutolea risiti na kutambua zimetajwa kuwa ni changamoto kubwa katika baadhi ya vituo jambo ambalo linawafanya abiria kusafiri bila kulipa.

Katika kituo cha kisutu  baadhi ya abiria walalamikia utaratibu huo wa kusafiri bila tiketi kwa madai kuwa kituo walichotoka mfumo wa ukatishaji tiket ulikwama na kuwaruhusu kupanda kwenye mabasi na kwenda kulipia kituo watakacho teremkia.

Tatizo la baadhi ya mashine kufeli kutambua tiketi limewafanya baadhi ya abiria kutumia mapungufu hayo kwa kutumia tiketi moja kwenye safari zake zote huku wengine wakilalamikia foleni ya kutoka kuwa kubwa baada ya mashine hizo kufanya utambuzi kwa muda mrefu.

Changamoto hizo zinapaswa kutafutiwa ufumbuzi na mamlaka husika kwani zinaweza kusababisha upotevu wa mapato katika mradi huo.

No comments:

Post a Comment