Monday, 23 May 2016

Hiki ndio kiasi kilichotolewa na serikali katika kujenga nyumba za walimu nchini.

Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni nne kwa ajili ya kujenga nyumba walimu kwenye shule za msingi 40 katika wilaya 40 i hapa nchini lengo likiwa kuipatia ufumbuzi changamoto ya baadhi walimu kukataa kuripoti kwenye vituo vya kazi wanavyopangiwa kwa madai ya kukosekana kwa  miundoimbinu rafiki katika shule husika .

Akiongea na waandishi wa habari juu ya  miradi ya ujenzi wa nyumba hizo za walimu ambazo zitakua zinabeba familia sita kwa kila nyumba zikiwa na umeme jua na runinga, meneja wa mawasilaiano na uhusiano  mamlaka ya elimu Tanzania SYLVIAN  Lupembe amesema ujenzi huo utakamilika ndani ya mwaka huu wa fedha ambapo amedai utaweza kuongeza ufanisi kwa walimu na ufaulu kwa wanafunzi.

Wakiongea na channel ten kaimu afisa elimu msingi kutoka  halmashauri ya mpwapwa Alexander Kiohi amesema mbali na kuwepo kwa tatizo la walimu lakini baadhi ya shule walimu wamekua wakigoma kwenda kuripoti kutokana na kukosekana kwa miundo rafiki huku mwalimu mkuu wa shule ya msingi mbuga ambapo  ujenzi wa nyumba hiyo unafanyika Omary Mbwana  amesema eneo hilo linakosa hata nyumba za kupanga ili walimu waweze kuripoti shuleni hapo.

No comments:

Post a Comment