Saturday, 21 May 2016

Hii ndio sentensi nne za Zitto Kabwe kuhusu Rais Magufuli

Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama cha ACT 
Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa 

Rais Magufuli ameonyesha kuwa hataki mchezo kwenye serikali 
yake 
baada ya jana kutengua nafasi ya Waziri wa Mambo ya Ndani.

Rais Magufuli jana ametengua uteuzi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Charles Kitwanga baada ya kuingia bungeni na kujibu swali linaloihusu wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa. Zitto Kabwe amedai kuwa kitendo kilichofanywa na Rais ni kama kutuma salamu kwa watendaji wake kuwa hataki mchezo.

Zitto Kabwe
"Uamuzi wa Rais kumfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani unatuma ujumbe mmoja kuwa hataki mchezo. Rais amethibitisha kuwa anao uwezo wa kutumbua hata aliowateua. Ni maamuzi muhimu sana kwa Kiongozi wa aina yake. Wale vijana waliokuwa wanatumwa kumtetea wasimame kumtetea. Rais kaonyesha Uongozi 'no nonsense'" 

No comments:

Post a Comment