Saturday, 21 May 2016

Aliye kuwa mkurungenzi wa jiji la Dar es salaam Wilson Kabwe kuagwa Jumanne wiki ijayo.

Marehemu Wilson Kabwe enzi za uhai wake akiwa ofisini.

Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo, utaagwa siku ya jumanne ya juma lijalo nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirisha kuelekea Same Mkoani Kilimanjaro.

Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo ,utaagwa siku ya jumanne ya juma lijalo nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirisha kuelekea Same Mkoani Kilimanjaro kwa maziko. 

Mhe. Isaya Mwita amesema marehemu Kabwe alifariki dunia jana baada ya kuugua kwa muda mrefu tangu mwaka jana na alikwenda India mwezi wa pili kwa matibabu na baadaye alirejea nchini mwezi wa nne ikiwa afya yake imeimarika, lakini baadaye alilazwa katika hospitali ya Mama Ngoma Mwenge hadi umauti ulipompata.

Rais Dkt. John Magufuli alimsimamisha kazi marehemu Wilson Kabwe Aprili 19 mwaka huu wakati akizindua daraja la Kigamboni kutokana na ufisadi wa kutisha katika utekelezwaji wa mikataba mitatu, inayohusu maeneo ya ukusanyaji mapato ya Stendi Kuu ya Mabasi Yaendayo Mikoani ya Ubungo na kodi ya uegeshaji magari katikati ya mji na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi Bilioni 3.

Kabla ya kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam marehemu Kabwe ameshawahi kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, na ndipo baadaye alipohamishiwa Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment