Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) kimesema kuwa kinaunga mkono uamuzi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Charels
Kitwanga kwani kiongozi wa umma kuingia bungeni akiwa amelewa si sahihi na haileti picha nzuri kwa wanachi wanaowategemea wao kama watunga sera wa nchi.
Akiongea na East Africa Radio Mwenyekiti wa CHAUMA Bw. Hashim Rungwe ameitoa kauli hiyo na kuongeza kuwa baadhi ya viongozi wanawakatisha tamaa sana wananchi kwani watanzania wanawategemea wao kupanga mipango itakayoiletea nchi maendeleao lakini badala yake wanaingia bungeni wamelewa ilihali wizara yake inawasilisha bajeti.
Aidha, Bw. Rungwe amemtaka rais kuendelea na mapambano ya kuondoa umasikini unaoonekana kuwakandamiza watanzania kwa kiasi kikubwa na njia pekee ya kuwakomboa ni kutengeneza mazingira ya kuwapatia ajira na kuboresha mazingira ya kilimo na biashara ili vijana wengi waweze kujiajiri.
No comments:
Post a Comment