Asilimia kubwa ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi nchini yameendelea kuathiri zaidi vijana tofauti na makundi mengine katika jamii ambapo ushamiri zaidi ukijitokeza kwa vijana wa kike ikilinganishwa na vijana wa kiume.
Hayo yamebainishwa jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa tume ya taifa ya kudhibiti ukimwi TACAIDS Dk, Fatuma Mrisho wakati wa uendeshaji wa harambee ya uchangiaji wa fedha za kupanda mlima Kilimanjaro kwa ajili kuendeleza mapambano dhidi ya ukimwi kwa mwaka 2016.
Dk.Mrisho amesema kwamba Wasichana wana uwezo wa kupata maambukizi mara mbili zaidi ya wavulana ambapo kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa viashiria vya VVU na malaria 2011/2012, kiwango cha maambukizi ya virusi vya UKIMWI miongoni mwa wasichana ni asilimia 6.6 wakati wavulana ni asilimia 2.8. Vijana wa kike walio katika hatari ni wale wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24 wakati wavukana ni kati ya miaka 23 hadi 24.
Kwa upande wake waziri Waziri ofisi ya makamu wa rais anayeshughulikia muungano na mazingira Januari Makamba amesema serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na mashirika, makampuni pamoja na sekta binafsi na itaendelea kuunga mkono juhudi hizo ili kuleta maendeleo kwa wananchi na huduma za karibu
No comments:
Post a Comment