Sunday, 22 May 2016

Hii ndio Taarifa ya Ripoti ya chama cha CUF Kuhusu uvunjifu wa haki za binadamu.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui
Chama cha wananchi Cuf leo kimezindua Ripoti ya Uvunjifu wa Haki za Binadamu unaodaiwa kufanywa na Vyombo vya dola ikiwemo jeshi la Polisi kati ya mwaka 2015 kabla ya Uchaguzi mkuu october 25,na 2016 baada ya Uchaguzi wa marudio visiwani zanzibar.

Akizunza na waandishi wa habari jijini dsm Naibu katibu Mkuu wa Chama cha wananchi Cuf Visiwani zanzibar Nassor mazrui amesema ripoti hiyo imebainisha Vitendo vya Uvunjifu wa haki za binadamu ambapo pia ripoti hiyo itasambazwa katika mashirika na taasisi za haki za binadamu ndani na nje ya nchi huku Chama hicho kinatarajia kufungua kesi mahakama kuu dhidi ya Jeshi la Polisi na wizara ya mambo ya ndani ya Nchi.

Aidha bw,Mazrui amesema Ripoti hiyo pia wanatarajia kumkabidhi rais  Dr.Magufuri huku pia wakifanya utaratibu wa Kufungua kesi katika mahakama ya kimataifa ya ICC 

No comments:

Post a Comment