Sunday, 22 May 2016

Serikali yatoa siku 21 kwa benki hizi jijin Dar es salaam kuweka wazi majina ya watumishi hewa.

Serikali ya Mkoa wa Dar essalaam Imetoa siku 21 kwa  benki sita katika jiji la dsm kushirikiana na Mkoa kutoa majina ya watumishi hewa waliokuwa wakichukua fedha kupitia Benki hizo baada ya Kuzingizwa kutoka hazina kwa ajili ya Mishahara hewa  au kuwajibika kuzikabidhi  fedha hizo zinazofikia shilingi billion 3.million 664.

Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul Makonda akizungumza na waandsihi wa habari jijini dsm amesema pamoja na agizo hilo pia ametaka kusitishwa na kufungwa akaunti 283 zilizokuwa zikitumika kulipia watumishi hewa.

Ameitaja benki sita ni NMB ambayo zilipitishwa shilingi bilion 2.867.4, CRDB milion mia nne na Mbili 329,888,NBC 141,412 34. DCB  Milioni 85,111.418 Sarndar Charter..Milion 2,na Elfu 40 pamoja na Comunity bank milion 196 .666. ambapo Mkuu huyo alitoa maagizo yafuatayo.

Aidha Bw,Makonda amesema kesho atakutana na wakuu wa Idara zote za jiji la dsm ili kuanza kuingia makubaliano ya mkataba waliosaini kubaini watumishi hewa huku akibainisha kuwa muda waliopewa unatosha na ikibainika watumishi hewa mkuu wa idara husika atawajibika kulipa gharama zote za fedha zilizopotea pamoja na kufikishwa mahakamani kwa Uhujumu Uchumi.

No comments:

Post a Comment