Manispaa ya Kigoma Ujiji inazalisha tani 171 za taka, lakini halmashauri ina uwezo wa kuzoa tani 30 tu, hali inayosababisha kuzagaa kwa uchafu, kuziba mitaro ya majitaka,kuwepo kwa harufu kali na uharibifu wa vyanzo vya maji,
Sultan Ndoliwa ni kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma ujiji ambapo anaeleza changamoto ya uzalishaji wa taka katika eneo lake ni mkubwa na kusababisha kushindwa kufikia lengo la uzoaji wa taka kwa siku kutokana na uchakavu wa miundombinu ya usafiri.
Kuzagaa kwa taka hizo kunasababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara, vyanzo vya maji, harufu kali na kuziba kwa mifereji inayosafirisha maji na kupeleka katika ziwa Tanganyika ambapo maji hayo hutumika kwa matumizi ya wakazi wa mkoa huo na hivyo kuhofia usalama wa afya zao kutokana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
Halmashauri ina uwezo wa kuzoa taka tani 36 huku tani 171 zinazalishwa kwa siku jambo linalochangia uzagaaji wa taka katika maeneo mbalimbali na hivyo jamii inatakiwa kutoa mchango mkubwa katika kuhakikisha uzalishaji huo unapungua kwa baadhi ya taka kuchomwa katika maeneo wanayoishi.
No comments:
Post a Comment