Sunday, 22 May 2016

Waziri mkuu Majaliwa atoa neno hili kuhusu Waziri kitwanga kutumbuliwa na Raisi Magufuli.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kumsimamisha kazi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi ni uamuzi sahihi kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma.

Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano maalum na kipindi cha Nipashe kinachorushwa na Radio One jijini Dar es salaam.

''Rais amezingatia sheria ya utumishi wa umma kwamba mtumishi anayebainika kulewa wakati wa kazi husimamishwa kazi hivyo sheria hiyo ndiyo ambayo Rais ameitumia ukizingatia Waziri alikuwa akijibu swali nyeti lililohusu wizara yake''

Waziri Mkuu ameongeza kuwa pombe inaruhusiwa kwa mujibu wa taratibu na mtu anaweza kunywa nyumbani aupopote kwa kuzingatia sheria lakini kuwa mlevi wakati wa kazi ni kinyumbe na sheria za umma.

Rais Juzi alimsimamisha kazi Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga kwa kujibu swali la Mbunge wa Mlimba Suzan Kiwanga (CHADEMA) huku akiwa amelewa na kujibu kwa utani.

Mbunge huyo aliuliza kuhusu makazi mabovu ya askari polisi katika wilaya ya Kilombero hususani jimbo lake la Mlimba ambapo alitaka pia kujua ni lini serikali itamaliza tatizo hilo.

Katika majibu ya Waziri Kitwanga pamoja na kuonyesha kwamba serikali ina upungufu wa nyumba elfu kumi za pilisi aliongeza majibu kwamba serikali itafanya linalowezekana kumaliza tatizo hilo nna kuhusu miaka mingapi Kitwanga alimuuliza Mbunge huyo kwani wewe una miaka mingapi?

No comments:

Post a Comment