Tuesday, 17 May 2016

Kauli ya serikali kuhusu sakata la Lugumi hii hapa.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Charles Kitwanga

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Charles Kitwanga, amesema serikali imetoa ushirikiano wa kutosha kwenye kamati zote zilizowaita juu ya sakata la Mkataba wa ufungaji wa mashine za kuchukulia alama za vidole maarufu kama mkataba wa Lugumi.



Waziri Kitwanga amesema hayo jana Nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya waandishi kumuuliza ni kwanini Serikali haijawasilisha taarifa ya mkataba wa Lugumi katika kamati kama ilivyotakiwa.

Mhe. Kitwanga amesema Jeshi la Polisi limeeleza ukweli uliopo juu ya sakata la Mkataba wa huo wa Lugumi na kusema kuwa sulala hilo pia aliliwasilisha kwenye kamati ya Ulinzi na usalama.
Wizara hiyo katika uwasilishaji wa bajeti yake imeomba jumla ya shilingi bilioni 860 kwa ajili yas utekelezaji wa majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ili kufanikisha usalama wa nchi na raia wake kwa kiwango kikubwa.

Nao baadhi ya wabunge wametoa maoni yao kuhusu Bajeti ya wizara hiyo na Jeshi la Polisi ambapo Mhe. Zitto Zuberi Kabwe alionyesha kuwa na imani na Kamishna mpya wa Kikosi cha Zimamoto kuwa anaweza kuleta mabadiliko katika jeshi hilo.

No comments:

Post a Comment