Wednesday, 11 May 2016

Kauli za watumiaji wa Daraja la Nyerere kuhusu viwango vya Nauli hii hapa

 
Baada ya Serikali kutangaza viwango vipya vya tozo jana vitakavyotumika katika daraja la Mwalimu Julius Nyerere lililopo jijini Dar es salaam, baadhi ya watumiaji wa daraja hilo wamekubaliana na viwango hivyo na kuishukuru Serikali kwa kuwarahisishia usafiri.

 Baadhi ya wananchi na watumiaji wa daraja hilo wamesema kuwa uwepo wa daraja hilo umesaidia kuondoa kero mbalimbali za usafiri ikiwemo msongamano wa foleni uliokuwa unajitokeza kwenye vivuko vya magogoni na kigamboni, hali ambayo ilisababisha kuzorota kwa shughuli mbalimbali za kikazi na biashara.

Aidha wananchi hao wameongeza kuwa viwango vya tozo vilivyowekwa na serikali vimefuata na kuzingatia hali ya maisha ya Mtanzania kuanzia maisha ya chini na ya kati, hivyo kila mtumiaji wa daraja hilo atakuwa na uwezo wa kumudu gharama hizo.

Katika hatua nyingine watumiaji wa daraja hilo wametakiwa kulitunza daraja hilo ili liweze kudumu huku suala la usafi na usalama likizingatiwa na kufuatwa vyema.

No comments:

Post a Comment