Monday 2 May 2016

Ligi Kuu Tanzania bara kuendelea kesho Yanga na Stand United kucheza

Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara inaendelea tena hapo kesho kwa mchezo mmoja kupigwa ambapo mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga watakuwa ugenini dhidi ya Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Yanga imeendelea kujichimbia kileleni mwa Ligi Kuu baada ya kuifunga Toto Africans ya jijini Mwanza kwa magoli 2-1 uwanja wa CMM Kirumba mwishoni mwa wiki, huku ikiziacha Azam FC na Simba ambazo hapo jana zilitoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bila kufungana.

Mara baada ya mchezo huo, Yanga itarejea Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wake wa awali wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Sagrada Esperanca ya Angola utakaochezwa Mei 07 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment