Monday, 2 May 2016

TPA Kuboresha Bandari ya Dar es salaam

Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania TPA imetangaza kuanza kufanya maboresho ya bandari ya Dar es salaam ili kuondokana na msongamano wa mizigo pamoja na kurahisisha upakuaji wa mizigo unayopitia katika bandari hiyo.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam,Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo,Mhandisi Aloyce Matey amesema kumekuwa na ongezeko la mizigo inayopitia katika bandari hiyo kwa miaka mitano mfululizo hali inayowalazimu kufanya marekebisho makubwa ili kuendelea kutoa fursa kwa nchi jirani kuendelea kutipisha mizigo katika Bandari ya Tanzania.

Mhandisi Matey amesema bandari ya Dar es salaam inakabiliwa na uchakavu wa Miundombinu na kuwa na kina kifupi cha maji cha mita 9 na ufinyu wa lango la kuingilia meli lenye upana wa mita 140 ambalo linaruhusu meli zenye urefu usiozidi mita 243 tu kuingia na meli kubwa zaidi zinashindwa kuingia.

Kwa Upande Mwingine,Msimamiz wa Mamlaka ya Bandari Mhandisi Marry Myaya amesema bandari ya Dar es salaam imefunga vifaa vya kupimia mafuta yanayopakuliwa katika Bandari hiyo kabla ya kufikishwa katika maghala

No comments:

Post a Comment