Monday 2 May 2016

Wafanya biashara ndogo ndogo Ubungo Waondolewa katika eneo hilo

 Mkurugenzi wa Biashara Manispaa ya Kinondoni amesema wafanyabiashara walioondolewa maeneo ya Ubungo Tanesco, hawataruhusiwa kurejea tena eneo hilo na badala yake wametakiwa kwenda eneo la Simu 2000 ambapo maeneo maalum yametengwa kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo yaani wamachinga.

 Eneo la Ubungo Tanesco ambako Manispaa ilikuwa inamalizia kubomoa vibanda vya wafanyabiashara, mkurugenzi huyo amesema hatua hiyo ni matayarisho ya ujenzi wa barabara ya juu, ambayo itasaidia kupunguza msongamano jijini Dar es salaam.

Kwa upande wao, baadhi ya wafanyabiashara wa soko hilo lisilo rasmi, wamesema waliitikia wito wa meya wa manispaa hiyo kuelekea kituo cha simu 2000,lakini wameshindwa kuendelea kukaa huko kutokana na ukosefu wa maeneo ya kufanyia biashara kwani vizimba vyote vimejaa japo manispaa ilidai kuwa nafasi ipo.

No comments:

Post a Comment