Miongoni mwa masharti yaliokuwapo katika kiapo hicho ni kwamba iwapo ikigundulika kuwapo kwa watumishi hewa katika idara husika baada wiki moja ijayo,Afisa utumishi au mkuu wa idara hiyo atalipa gharama za mishahara iliyopotea,kushitakiwa kwa uhujumu uchumi,kuachishwa kazi lakini pia kufikishwa mahakamani.
Hatua ya kusaini na kula kiapo inatokana na baadhi ya wakuu wa idara pamoja na maafisa Utumishi katika jiji la DSM kudaiwa kutoa taarifa za uongo kwa Mkuu wa mkoa Paul Makonda na wakuu wa wilaya za jiji hilo baada ya kutoa idadi ndogo ya watumishi hewa kwa mkoa wa dsm ambao walikuwa 74 tu, huku uhakiki wa sasa uliofanywa na tume maalum ukibaini watumishi hewa 209 ambao wametafuna kiasi cha takribani shilingi bilion 2.7
Kiapo hicho cha kazi kiliionekana kuwa mwiba kwa watumishi hao wa mkoa wa DSM kutokana na wengi wao kushindwa kujaza,huku wakileta hoja ambazo zilionekana kutokuwa na nguvu kwa mkuu wa mkoa kwa kuogopa kujifunga mpaka pale Bwana Makonda alipotoa dakika 5 kujaza na kuwasilisha.
Baadhi ya wakuu wa idara pamoja na maafisa utumishi wamesema kiapo hicho ni kizuri kwa ajili ya Utendaji kazi lakini ni mwiba kwa wakuu wa idara hasa kutokana na wengi wao kufanya kazi kwa mazoea, huku Katibu tawala wa mkoa wa Dsm THERESIA MBANDO akikiri kuwepo kwa taarifa zenye utata juu ya idadi ya watumishi hewa
No comments:
Post a Comment