Wednesday 11 May 2016

NACTE kusitisha Matumizi ya Mfumo wa Udahili wa CAS


Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi NACTE limesisitiza matumizi ya mfumo wa udahili wa pamoja CAS kwa wanafunzi wote wanaojiunga na programu mbalimbali za elimu na mafunzo katika vyuo vyote vya umma na binafsi nchini.


Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk. Adolf Rutayuga amesema serikali imeweka utaratibu huo ili kuondoa udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wanafunzi ama vyuo katika kudahili wanafunzi wasio na sifa kwa ajili ya kujiunga na vyuo hivyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mkutano wa wakuu wa vyuo vya umma nchini, Dk. Rutayoga amesema mfumo wa CAS unaotekelezwa NACTE kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo vikuu umeanza rasmi Machi mwaka huu, na unatarajia kuendelea hadi Septemba mwaka huu, na ndio utakaokuwa ukitumika siku zote.

Mfumo wa kuwa na kituo cha Udahili wa pamoja CAS kinaondoa utaratibu wa zamani wa wanafunzi kuomba fomu kwenye vyuo walivyokusudia kwenda kusoma.

No comments:

Post a Comment