Wednesday 11 May 2016

Mbunge bashe akosoa hotuba ya Waziri Mwijage kwa kusema haya


Akichangia hotuba ya bajeti Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Bashe amesema kuwa hotuba za wizara hizo zimejielekeza katika maeneo ambayo siyo kipaumbele kwa wananchi walio wengi.

Ripoti ya kamati ya viwanda na biashara na katika miradi ya mikakati ya ya kipaumbele ni pamoja na kufufua General Tyre na serikali imetenga bilioni mbili na kamati inasema ili kuifufua General Tyre ni bilioni 60 wakati bajeti ya wizara hii ni bilioni 80 sasa sijui Waziri anakwenda kufanya muujiza gani.

''Kama tunakaka kuuondoa umaskini wa nchi ni wapi pa kuanzia Engaruka, General Tyre? Namtakia heri Kaka yangu Mwijage kila la kheri ili tuone huo muujiza mwaka kesho, kwenye Bunge lililopita tulisema 65% ya wananchi wetu wapo kwenye sekta kilimo kwa nini hatujasema kwamba tungewekeza kwenye viwanda vidogo vidogo vya kusindika bidhaa?''-Amesema Bashe.

Bashe ameongeza kuwa Mpango wa Serikali wa mwaka mmoja unabainisha wazi kwamba umelenga kufungamanisha maendeleo ya viwanda na watu sasa mimi nahoji tutawezaje kufungamanisha maendeleo ya viwanda na watu na hatuwekezi kwenye pamba, korosho, katani, alizeti hatuwekezi popote halafu tunatarajia miujiza?

''Nimeangalia hotuba ya Waziri wa Kilimo na Uvuvi Mwingulu Nchemba nimeangalia Hotuba ya Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage nimekata tamaa'' We are Planning to fail' hatuwezi kujadili kufanya mabadiliko ya uchumi bila kuamua kuweka vipaumbele vya maeneo yanayogusa watu, tutakuja hapa kusema uchumi umekua kwa asilimia 8 wakati watu wetu ni masikini kwa sababu mipango yetu yote inaacha watu wetu nje.

No comments:

Post a Comment