Thursday 12 May 2016

Serikali yakutana na wadau kwa ajili ya kujenga viwanda katika mradi wa gesi nchini.

 
Serikali imekutana na wawekezaji wakubwa wa makampuni yanayotekeleza miradi ya kuuza gesi ya kimiminika (LNG) ili kuwezesha taifa kuweza kuuza nje ya nchi nishati ya gesi asilia.

Uamuzi huo wa serikali ni katika mchakato wake wa kuhakikisha Tanzania inafanikisha ujenzi wa mradi mkubwa wa
kiwanda cha kubadilisha gesi asilia kuwa kimiminika na hatimaye kuwa rahisi kusafirishwa popote duniani, kiwanda kitakachogharimu zaidi ya dola za kimarekani bilion 60.


Katika Kongamano la siku mbili lililohusisha wadau wa mafuta na gesi asilia kutoka maeneo mbalimbali duniani, wawekezaji hao wamekubaliana na serikali kuangalia sheria na taratibu zitakazotumika katika kuongoza na kufanikisha utekelezaji wa mradi huo unaokusudiwa kutekelezwa mkoani Lindi.

Akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kukamilika kwa kongamano hilo la siku mbili lililoratibiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC, mkurugenzi wa TPDC wa Uzalishaji, Usafirishaji na usambazaji wa Gesi asilia Dk WELLINGTON HUDSON amesema licha ya kwamba bei ya gesi ya kimiminika imeshuka kwenye soko la dunia, bado uwekezaji wa aina hiyo ni muhimu kwa siku za baadae kwa taifa.

Kiasi cha gesi asilia kilichogundulika Tanzania ni futi za ujazo trilion 55.08.

No comments:

Post a Comment