Monday, 2 May 2016

Tazama Kauli ya Waziri Kigwangalla kuhusu mashine za Ocean Road

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema kwamba serikali inatambua matatizo wanayokumbana nayo wananchi hospitali ya matibabu ya saratani nchini Ocean Road Jijini Dar es salaam.
Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tumbe visiwani Zanzibar Rashid Ali Abdalla aliyetaka kujua kama serikali itafahamu adha wanayokumbana nayo wananchi katika hospitali ya Ocean Road kutokana na uhaba wa mashine pamoja na huduma kutotia matumaini.

''Serikali inatambua sana tatizo la Ocean Road na waziri mwenyewe alipofika pale alilia machozi na kwa tatizo lililopo serikali imekubali kutenga bilioni 4 kwa ajili ya kununua mashine mpya za linear accelerator na CT simulator ambapo hadi sasa bilioni 2.5 zimeshapatikana ilikununua mashine hizo''. Amesema Kigwangalla.

Aidha Naibu Waziri amesisitiza kuwa hospitali hiyo kwa sasa haina mashine mbovu kwani zilizopo zinafanya kazi na zitakaponunuliwa hizo nyingine zitasaidia sana kupunguza tatizo la msongamano wa wagojwa hospitalini hapo.

No comments:

Post a Comment