Sunday 15 May 2016

TEWUTA imeiomba serikali kuchunguza kesi hizi kwa kampuni hizi za simu nchini.

Screen Shot 2016-05-15 at 11.34.09 AM
Chama cha wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Mawasiliano Tanzania – TEWUTA

Kimeiomba serikali kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya tuhuma za ukandamizaji na unyonyaji wa wafanyakazi wanaofanya kazi Kwenye kampuni za simu za Viettel Tanzania limited inayomiliki Halotel na Kampuni ya Erolinki Tanzania.
Kwa mujibu wa Chama cha wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Mawasiliano Tanzania – TEWUTA,  ndani ya Kampuni ya Viettel Tanzania Limited inayomiliki Halotel, TEWUTA imedai kumekuwa na ubaguzi kwa wafanyakazi wazawa na wageni  sambamba na kuajiri watumushi wageni ambao wanafanya kazi zinazoweza kufanywa na wazawa, Hivyo TEWUTA imeiomba serikali kuifanyia ukaguzi kampuni hiyo ili kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, watendaji wakuu wa TEWUTA wameiomba serikali kusimamia sera zinazowaongoza wawekezaji wanapoingia nchini, na kuziomba wizara za Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano pamoja na Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu kufanya uchunguzi wa kina ili watakaobainika  kwenda kinyume na sheria za nchi wachukuliwe hatua za kisheria.

No comments:

Post a Comment