Tafiti zinaonesha kwamba asilimia kubwa ya magonjwa ya saratani kwa binadamu husababishwa na matumizi ya chakula au vinywaji ambavyo vina mabaki ya chembechembe za mionzi ya nishati ya nyuklia ambayo ilitupwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo baharini na maeneo ya jirani baada ya mlipuko wa kinu cha nguvu za nyuklia cha Chernobyl nchini Ukraine miaka 30 iliyopita.
Kufuatia Mkasa huo ambao unatajwa kuacha sumu ya kudumu itokanayo na chembechembe za mionzi ya nyuklia katika maeneo mbalimbali ,Shirika la nguvu za atomic duniani liliweka utaratibu wa kuhakikisha vyakula vyote vitokanavyo na nafaka ,nyama na vinywaji vinapimwa kabla ya matumizi yake ,shabaha ikiwa ni kubaini uwepo wa mabaki ya mionzi ya nyuklia au laa. ambapo kwa Tanzania jukumu hilo liko chini ya tume ya nguvu za atomic
Ni katika jumba hili ambalo ndipo sampuli za shehena zote za vyakula,sukari,mafuta ya kupikia, vinywaji na mbolea kutoka nje na sehemu nyingine ambazo hutiliwa shaka hufikishwa hapa na kufanyiwa vipimo vya kimaabara ili kulinda afya za walaji.
Mkurugenzi mkuu wa Tume ya nguvu za atomi nchini yenye makao yake makuu jijini hapa anawatoa wasiwasi waagizaji wa bidhaa zote ambazo zinatiliwa shaka kwa kuwa na uwezekano wa kuwa na mabaki ya mionzi ya nyuklia
No comments:
Post a Comment