Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wenye Albinism Bi. Ikponwosa Ero. |
Akizungumza
baada ya ziara yake rasmi ya kwanza nchini humo Bi. Ero amesema
walemavu wa ngozi huko Malawi wanaishi kwa hofu kubwa, hawalali na hata
hawaamini wale wanaopaswa kuwalinda kutokana na familia kuhusika katika
baadhi ya matukio ya wao kushambuliwa.
Bi. Ero amesema hali ni mbaya zaidi kwa kuwa tangu mwaka 2014 visa 65 vya mashambulizi dhidi ya albino viliripotiwa nchini Malawi ikiwemo visa viwili wakati wa ziara yake.
Amesema fikra potofu za matumizi ya viungo vya albino kwa ushirikina na kwamba albino hawafariki dunia bali wanatoweka zinahatarisha zaidi maisha yao.
Pamoja na kupongeza mpango wa serikali wa mwaka 2015 kulinda albino, bado ametaka mafunzo zaidi kwa polisi, waendesha mashtaka na mahakimu ili hukumu za kesi hizo ziendane na ukubwa wa tukio husika.

No comments:
Post a Comment