Monday, 2 May 2016

Jaji Mkuu wa Tanzania kuongoza maadhimisho ya siku ya habari


Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ambapo kitaifa inaadhimishwa jijini Mwanza.

Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, inayoadhimishwa Mei 3 kila mwaka duniani kote, ilianzishwa na Umoja wa Mataifa kusherehekea kanuni za uhuru wa habari na kuwakumbuka wale waliokufa wakati wakijaribu kutekeleza kanuni hizo. Siku hii hutumika kama jukwaa ambalo hutumiwa na wadau wa vyombo vya habari kushinikiza mataifa kutengeneza sheria rafiki za vyombo vya habari zinazoweza huhakikisha uhuru wa habari katika nchi zao. 

Mkutano huo pia utatoa nafasi ya kujadili na kushauriana kuhusu maana ya sheria ambazo serikali imezipitisha na kuwasilishwa kwa mara ya kwanza katika Bunge mwaka jana. Zinajumuisha Sheria ya Makosa ya Mtandao, Sheria ya Takwimu, Muswada wa Huduma ya Habari na Sheria ya Upatikanaji wa Habari. 

Aidha wageni wengine mashuhuri watakaohudhuria mkutano huo ni pamoja na Wageni wengine mashuhuri watakaohudhuria maadhimisho hayo ni pamoja na Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Wasanii, Mhe. Nape Nnauye (mbunge), Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, mh. Alvaro Rodriguez, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) mh. Roeland van de Geer, Mwakilishi Mkazi wa UNESCO Zulmira Rodrigues, na Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi, pamoja na wadau 250.

No comments:

Post a Comment