Thursday, 19 May 2016

Waziri mkuu atoa katazo hili kwa wakulima nchini.

Waziri Mkuu ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa viti Maalumu CUF Saumu Sakala aliyeuliza swali kwamba wafanyabishara wanaofunga rumbesa huikosesha serikali mapato na kuwanyonya wakulima serikali inatoa kauli gani?

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amesema ni kweli wapo wafanyabiashara wanaonunua mazao kwa rumbesa na serikali ilishatoa maagizo kuhusiana na jambo na inanekana yamekiukwa.

Waziri Mkuu ameagiza wakala wa vipimo nchini kuhakikisha jambo hilo linafanyiwa kazi na kuhakikisha magunia yanapimwa na vijijini kuhakikisha yanajazwa katika ujazo wake wa kawaida na si rumbesa.

Aidha Waziri Mkuu amewataka wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini kwa kuwa wao ni wakuu w ulinzi na usalama katika maeneo yao kuhakikisha wanashiriki kukomesha jambo hilo ili serikali iweze kupata mapato na wakulima waweze kunufaika na mazao yao.

No comments:

Post a Comment