lakini wamefuzu kwa matokeo ya jumla Sagrada Esparenca 1-2 Yanga hivyo kikosi hicho cha mabingwa wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara wananasonga mbele kwenye michuano hiyo ya Afrika.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa wa Madagascar, Hamada el Moussa Nampiandraza, aliyesaidiwa na Velomanana Ferdinand Jinoro na Jean Thierry Djaonirina, hadi mapumziko, tayari wenyeji walikuwa wamekwishajipatia bao lao hilo.
Bao hilo lilifungwa na mkongwe Arsenio Sebastiao Cabungula maarufu kama ‘Love Kabungula’ dakika ya 25, baada ya mabeki wa Yanga kufanya uzembe kidogo.
Mechi ya Yanga dhidi ya Esparanca haikuwa rahisi kwasababu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika wachezaji wanne wa Yanga walikuwa tayari wameoneshwa kadi za njano.
Haruna Niyonzima, Thabani Kamusoko, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Mlinda mlango Deogratius Munishi Dida ni baadhi ya wachezaji waliooneshwa kazi za njano kutokana na matukio tofauti ya kinidhamu.
Kipindi cha pili, Yanga waliachana na mchezo wa kujihami na kufunguka kuanza kushambulia, hali ambayo ilipunguza kasi ya wapinzani wao ambapo katika dakika ya 72 mshambuliaji Mzimbabwe Donald Ngoma alipoteza nafasi nzuri ya kufunga.
Kipa Deo Munishi 'Dida' aliweza kuokoa penati iliyotolewa baada ya Nahodha Nadir Cannavaro kumuangusha mchezaji wa Sagrada Esperanca.
Refa aliongeza dakika tano baada ya kutimia dakika 90 na Nahodha Cannavaro akatolewa kwa kadi nyekundu pia.
Vurugu zikaibuka dakika ya mwisho ya dakika za nyongeza na kipa wa Yanga, Dida akapigwa jiwe na mchezo kusimama kwa muda ambapo askari Polisi waliingia uwanjani kutuliza fujo na mchezo ukaendelea kwa sekunde kadhaa kabla ya refa kumaliza
No comments:
Post a Comment