Sunday 26 June 2016

Hii ndio kauli ya Rais Magufuli kwa BAKWATA na waumini wa dini ya Kiislam nchini.


Rais Dk. JOHN MAGUFULI amewahimiza viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania- BAKWATA na waumuni wa dini ya kiislam waendelee kuombea amani ya taifa pamoja na kukemea ipasavyo vitendo vya uhalifu katika jamii ya Kitanzania.


Kauli hiyo ya Rais imetolewa na Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN kwa niaba ya Rais katika halfa ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania- BAKWATA- katika uwanja wa shule ya sekondari ya KINONDONI MUSLIM jijini Dar es Salaam.

Amesema jamii yeyote inayolelewa na kukua katika misingi ya kufuata maandiko ya Mwenyezi Mungu ni vigumu kujiingiza kirahisi katika vitendo vinavyomchukiza Mwenyezi Mungu vikiwemo vya uhalifu.

Aidha amewatakia kheri waumini wote wa dini ya kiislamu kote nchini katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
SAMIA SULUHU HASSAN Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kwa upande wake, Mufti wa Tanzania Sheikh ABUBAKAR ZUBEIR ameipongeza serikali kwa hatua inazochukua katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu hapa nchini na kusisisita kuwa Viongozi wa BAKWATA wataendelea kushirikiana na serikali katika kukemea vitendo viovu katika jamii kama hatua ya kuhakikisha vitendo vya uhalifu vinatokomezwa nchini.

Mufti wa Tanzania pia ametoa rai kwa waislamu wote nchini wadumishe umoja, upendo na mshikamano miongoni mwao katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na baada ya mfungo kama kitabu kitukufu cha QUR’AN kinavyoelekeza.

No comments:

Post a Comment