Monday 13 June 2016

Hii ndio kauli ya serikali kuhusu askari wasiopigia saluti wabunge.



Serikali imewaagiza askari wa majeshi yote nchini kuzingatia kanuni za maadili yao ya kazi ikiwemo kupiga saluti kwa viongozi wote wakiwemo wabunge.
Agizo hilo limetolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole-Nasha wakati akijibu swali la nyongeza kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani la mbunge wa viti maalum kutoka Zanzibar Fakharia Shomari aliyetaka kujua ni kwanini askari wa jeshi la polisi hawapigi saluti kwa wabunge.

Katika maelezo yake, Ole Nasha amesema kuwa askari wote nchini ni lazima wazingatie taratibu hizo, na kwamba wanapaswa kupiga saluti kwa wabunge kila wanapowaona, na endapo hawatafanya hivyo, watakumbana na adhabu za kijeshi.

Ametaja baadhi ya adhabu watakazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na kukatwa mshahara, kufanyausafi wa mazingira, kuondolewa kikosini kwa muda n.k. na amewataka wabunge ambao hawatapigiwa saluti, kuripoti haraka mahali husika.

Akiongozea majibu hayo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi amesema agizo hilo linakwenda hadi kwa askari wa makampuni binafsi ya ulinzi ambao mara nyingi hupuuza kutoa heshima hiyo kwa viongozi hususani katika mabenki.
Sikiliza hapa majibu hayo…..

No comments:

Post a Comment