Monday 22 August 2016

Mkuu wa Mkoa wa PWANI Mhandisi Evarist Ndikilo atumbua watumishi hawa katika wilaya ya Mkuranga.

Mkuu wa mkoa wa PWANI Mhandisi EVARIST NDIKILO
Mkuu wa mkoa wa PWANI Mhandisi EVARIST NDIKILO amewasimamisha kazi watumishi wawili wa idara ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya MKURANGA kwa matumizi mabaya ya ofisi.

  Watumishi hao wanadaiwa kutumia vibaya ofisi wakati wa mchakato wa kuchukua  Ekari 30 za  shamba linalomilikiwa kisheria na taasisi  YOUTH WITH A MISSION TANZANIA lililopo katika kijiji cha KISEMVULE .

Mhandisi NDIKILO pia amesitisha mchakato uliofanywa  na watumishi hao wawili wa idara ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya MKURANGA katika kuchukua eneo hilo  hadi serikali itakapojiridhisha jinsi mchakato huo ulivyoendeshwa.
Mkuu huyo wa mkoa wa PWANI Mhandisi EVARIST NDIKILO amesema kuwa matumizi mabaya ya ofisi yaliyofanywa na Watumishi hao yamesababisha Halmashauri ya wilaya ya MKURANGA kulipwa Shilingi Milioni 450 bila Mkurugenzi  wa Halmashauri wala mhasibu  wa wilaya hiyo kufahamu.

Mhandisi NDIKILO ameigiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwahoji watu wote waliohusika katika mchakato huo na kumtaka Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya MKURANGA JUMA ABED kuwa makini katika utendaji wake wa kazi.

USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment