Monday, 22 August 2016

Waziri Mkuu Majaliwa atoa maagizo haya Kwa watendaji katika Mkoa wa Katavi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Katumba mkoani Katavi
Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amewataka watendaji wa Halmashauri Mkoani KATAVI kuwa makini na matumizi ya fedha za maendeleo.

Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amewataka watendaji wa Halmashauri Mkoani KATAVI kuwa makini na matumizi ya fedha za maendeleo zinazopelekwa katika maeneo yao.

Akihutubia wananchi katika Uwanja wa Azimio Wilayani MPANDA Waziri Mkuu MAJALIWA amesema Serikali imeanza kupeleka fedha za miradi ya maendeleo katika halmashauri mbalimbali hivyo ni vema kila mtendaji ahakikishe fedha hizo zinatumika kwa ajili ya ujenzi wa miradi iliyokusudiwa na si vinginevyo.

         Alisema ni lazima Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha viwango vya ubora wa miradi inayojengwa katika maeneo yao inalingana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa.

         Wakati huo huo Waziri Mkuu amemtaka Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, UMMY MWALIMU kwenda Wilayani MPANDA kuangalia namna ya kuipanua Hospitali ya Manispaa ya MPANDA ambayo inahudumia Mkoa wote wa KATAVI.

         Aidha amesema wakati mkoa ukiwa kwenye harakati za ujenzi wa hospitali ya mkoa wilaya nazo zianze ujenzi wa hospitali za wilaya ili kuhakikisha sera ya Serikali ya kuwa na hospitali katika kila wilaya inatekelezwa

USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment