Thursday 11 August 2016

Paul Mkonda atoa ufafanuzi huu kuhusu Walimu wote wa Mkoa wa Dar es salaam kusafiri bure.

144
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Mkonda ametangaza kuwa walimu wote wa Mkoa wa Dar es salaam watasafiri bure katika Treni zinazotoa Usafiri katika Jiji la dsm kwa kutumia Vitambulisho vya awali vilivyokuwa vikitumika kusafiria katika Usafiri wa mabasi ya Daladala huku wanafunzi watalipia Shilingi mia moja ktika usafiri huo wa Treni.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa na Mkurugenzi  mkuu wa Shirika la reli Tanzania Injinia Masanja Kadogosa amesema mpango huo umekubaliwa na Shirika la Reli baada ya mazungumzo na Bw,Makonda ikiwa ni jitihada za kuwapunguzia gharama za Usafiri kwa walimu wa Jiji la dsm.
Amesema mpango mwingine ambapo tayari ameshafikisha kwa Waziri mkuu majaliwa ni pamoja na walimu kusafiri bure katika mabasi ya mwendo kasi ambapo mazungumzo yanaendelea ili uanze baada ya makubaliano.
Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Reli Injinia Masanja kadogosa amesema Shirika hilo limezingatia maombi ya Bw,Makonda huku pia likiahidi katika kipindi kifupi kuleta treni za Kisasa zitakazotoa huduma katika jiji la Dsm baada ya maandilizi ya kusambaza miundombinu ya njia za Treni itakapokamilika.
Wakati huo huo Mkuu wa mkoa wa dsm amewataka wanachi wa Mkoa wa dsm kujitokeza kesho kumpokea Rais Dr.John Pombe Magufuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa akitoa mkoani mwanza ,ambapo pia wananchi wametakiwa kujipanga barabarani .

USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUTU FOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment