Tuesday 13 September 2016

Haya ndio makubaliano yaliofikiwa kati ya Klabu ya Azam FC na Simba FC kuhusu siku ya mechi na uwanja wataotumia.

Image result for azam fc vs simba
Uongozi wa klabu ya Azam FC umekubali kucheza mchezo wake wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara, dhidi ya Simba, kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Jumamosi hii.



Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Karume, jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa shirikisho hilo, Alfred Lucas, amesema TFF ilikaa na Azam, na timu hiyo, kuomba kuhamishia mchezo huo, kutoka uwanja wa Chamazi kuja uwanja wa Uhuru.

Pia Lucas, amesema kulikuwa kuna tetesi kwenye mitandao ya kijamii, kuwa mchezo huo, ungevurugika kutokana na kupanguliwa ratiba, kitu ambacho sio kweli.

USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment