Friday 18 November 2016

Taarifa kuhusu TRA kuongeza Muda wa Kuboresha Taarifa za Walipakodi.


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuwashukuru wakazi wa Dar es Salaam kwa  kushiriki katika zoezi la kuhakiki Namba ya Utambulisho Mlipakodi (TIN).

Kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi kutaka kuhakiki taarifa zao, Mamlaka imeamua kuongeza muda wa uhakiki hadi tarehe 31 Januari, 2017. Pamoja na kuongeza muda wa uhakiki, Mamlaka pia imeongeza vituo vya kuhakiki.

TRA pia inawakumbusha wananchi kuwa wale wenye TIN za biashara wanatakiwa kuhakiki katika ofisi za kodi Mkoa husika na wenye TIN zisizo za biashara (yaani TIN iliyotokana na maombi ya leseni ya udereva au ya kuingiza mzigo bandarini) wanaweza kuhakiki katika kituo chochote hapa Dar es Salaam.

Vituo vya uhakiki vilivyopo ni kama  ifuatavyo:
Pamoja na vituo hivyo, Mamlaka imeanzisha kituo kinachohama (Mobile Office) ambacho kinatoa huduma sehemu mbalimbali.  Ili kuongeza ufanisi, Mamlaka itaendelea kuboresha huduma zake kwa kuongeza vitendea kazi na vituo vingine vya kuhakiki.

Mwisho, Mamlaka inawasihi  wananchi kuepuka kutumia  Matapeli (Vishoka) kwani zoezi hili linamtaka mlengwa kufika mwenyewe kwenye kituo husika.

Kwa ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana na kituo cha huduma kwa walipakodi kwa kupiga simu za bure: 0800 780078 / 0800 750075 barua pepe: huduma@tra.go.tz


Pamoja Tunajenga Taifa Letu

Limetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA- Makao Makuu

USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

                              SUBSCRIBE ON YOUTUBE TIKISA TV

No comments:

Post a Comment