Thursday 3 November 2016

Waziri wa viwanda Mhe. Charles Mwijage asema kazi ya serikali ni "kupiga sound" si kujenga Viwanda.



Waziri wa maendeleo ya viwanda Mhe. Charles Mwijage amesema, kazi ya serikali ni kupiga sound wawekezaji waje wajenge viwanda, na si serikali kujenga viwanda, hivyo wizara yake imejitahidi kupiga sound na viwanda sasa vinajengwa.



Ameongea hayo kwenye kipindi cha maswali na majibu alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Godbless Lema lililoulizwa na Mhe. Khadija Ali kwa niaba yake lililomtaka kusema viwanda vitajengwa lini. "...nimepiga sound, wakaja kuwekeza..."alisema Mhe. Mwijage.

Mhe. Cecilia Pareso aliuliza swali la nyongeza kwa waziri wa viwanda lililokuwa na sehemu mbili:
(a) Ni lini serikali itafufua kiwanda cha general tire."tukiangalia bajeti, serikali ilitoa bilioni 60 kwenye wizara hiyo, lakini mpaka sasa ni bilion 2 tu zilizotolewa na serikali hii iliyofilisika, ni lini kiwanda cha general tire kitafufuliwa?"
(b)Lini wafanyakazi wanaokidai kiwanda cha general tire watalipwa?

Mhe. Mwijage alimtaka Mhe.Pareso amkabidhi nakala ya madai hayo, naye ameahidi kufuatilia madai hayo. Sambamba na hilo, Mhe. Mwijage aliendelea kusisitiza kuwa viwanda vinajengwa na kazi yake ni kupiga sound.

USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

                          SUBSCRIBE ON YOUTUBE TIKISA TV

No comments:

Post a Comment