Serikali imepiga marufuku mamlaka zake zote kutoa tamko,kulizungumzia, ama kulitolea ufafanuzi suala la Faru John hadi hapo taarifa rasmi ya Tume ya Waziri Mkuu itakapomaliza uchunguzi na kutoa ripoti.
Akiwa katika siku ya pili ya ziara ya kikazi wilayani Ngorongoro ambayo ililenga kukagua changamoto za uhifadhi Na kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya waziri mkuu naibu waziri wa maliasili na utalii Ramo Makani amesema kwa sasa hakuna mamlaka nyingine za serikali chini ya waziri mkuu zenye ruksa au mamlaka ya kutoa ripoti ya faru John zaidi yake kwa kuwa suala hilo bado linafanyiwa uchunguzi.
Wakati huo huo serikali imeunda kamati maalum ya kushughulikia mgogoro wa pori tengefu la Loliondo kwa kuwakutanisha wadau wote muhimu na wenye maslahi katika eneo hili ili kumaliza mgogoro huo sugu uliodumu kwa zaidi ya miaka thelathini.
Awali mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka amesema kamati hiyo inatarajiwa kuleta Mwanga Mpya wa Loliondo kwa kuwa nia ya serikali ni kuona mgogoro wa eneo hilo unamalizika kwa maslahi ya nchi,wananchi na wawekezaji huku mmoja wa wawekezaji katika pori hilo mkurugenzi wa OBC Izak Mollel akitoa angalizo kuhusu kamati hiyo.
Faru John aliyekufa akiwa na umri wa miaka 38 alihamishwa kutoka mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na kupelekwa katika eneo la Sasakwa Grumet Serengeti.
No comments:
Post a Comment