Serikali imezionya shule zote za sekondari na msingi nchini hususani za mashirika ya dini ambazo bado zinakaririsha wanafunzi darasa kwa kigezo cha kutofikia alama za ufaulu zilizowekwa na shule, kuacha kufanya hivyo kwa kuwa ni kinyume na sheria.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamishna wa Elimu nchini Nicolas Burreta imesema kuwa serikali kupitia wizara ya elimu imebaini kuwa bado kuna shule ambazo mbali na kukaririsha wanafunzi darasa, zimekuwa pia zikiwafukuza wanafunzi shule, na nyingine zikiwahamishia katika shule nyingine.
Kamishna Burreta katika taarifa hiyo ameziagiza shule hizo kufuta maagizo yao ya ama kuwakaririsha darasa, kuwafukuza wanafunzi hao, au kuwahamisha huku akiwataka wazazi ambao watoto wao wamefukuzwa au kuhamishwa, wawarudishe watoto wao katika shule hizo waendelee na masomo.
Pia amewataka wathibiti ubora wa shule, kanda wilaya na maafisa elimu wa wilaya na mikoa kusimamia agizo hilo na kwamba shule yoyote itakayokiuka maagizo hayo itachukuliwa hatua kali za kisheria.
No comments:
Post a Comment