Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema mshambuliaji wake Alexies Sanchez amepata majeraha kidogo na atakaa nje kwa wiki mbili.
Wenger amesema majeraha hayo yatamfanya Sanchez akose michezo ya mwanzoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu England ukiwemo mchezo wa Ijumaa ijayo dhidi ya Leicester City.
“Sanchez amepata majeraha kidogo na atakosa mchezo mmoja au miwili ya ligi, nafikiri ataanza kuukosa huu ujao dhidi ya Leicester.
“Hili ni pigo kwetu, ingawa naamini kuwa hakuwa tayari kucheza mchezo wa Ijumaa lakini ingekuwa vizuri kama angekuwa fiti,” alisema Wenger.
No comments:
Post a Comment