Serikali imesema haitasita kuwachukulia hatua Wakurugenzi wa halmashauri nchini ambao hawatekelezi maagizo ya serikali ikiwamo kutenga asilimia kumi ya mapato kwa ajili ya wanawake na vijana.
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera, bunge, kazi, ajira, vijana na watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusu siku ya kimataifa ya vijana duniani itakayofanyika mkoani Dodoma Agosti 12, mwaka huu.
Waziri Mhagama amesema fedha hizo kwa ajili ya makundi hayo zipo kisheria lakini baadhi ya wakurugenzi wamekuwa hawazitoi kwa walengwa.
Pia, waziri Mhagama amesema serikali haipo kwenye mchakato wa kufanya mapitio sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 kutokana na kupitwa na wakati.
Naye afisa vijana wa shirika linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA), Fatna Kiluvia, amesema Desemba mwaka 2015 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio namba 2250 ili kutambua idadi ya vijana na kubaini kuwa kundi hilo ni kubwa na linakua kwa kasi.
No comments:
Post a Comment