Wednesday, 9 August 2017

Beki wa Simba Zimbwe atoa kauli yake kuhusu ujio wa Niyonzima Msimbazi.

Image result for niyonzima simba
Beki wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein ‘Zimbwe’, ameibuka na kusema kuwa, kitendo cha kiungo raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima kujiunga na timu hiyo kwake kimemfurahisha, hivyo wapinzani wasubiri kuona makali yake uwanjani pindi ligi ikianza.

Zimbwe ameyasema hayo baada ya Simba kumtambulisha rasmi Niyonzima kuwa mchezaji wao akitokea Yanga aliyoitumikia msimu uliopita.

Kabla Niyonzima hajajiunga na Simba, Tshabalala ametamba kuwa, anatamani siku moja acheze na Mnyarwanda huyo ambapo sasa amepata fursa ya kucheza naye.

“Nilishawahi kusema kwamba natamani siku moja nicheze na Niyonzima kutokana na kwamba ni mchezaji mzuri na amekuwa msaada katika timu awapo uwanjani, nilimuona akifanya hivyo alipokuwa Yanga.


“Lakini nashukuru sasa nipo naye hapa Simba na msimu ujao tutacheza pamoja, hivyo wapinzani wasubiri maana watakoma, kila idara sasa imekamilika hapa Simba, kilichobaki ni ushindi kwa kwenda mbele,” alisema Tshabalala.

No comments:

Post a Comment