Wednesday, 30 August 2017

Kocha wa Simba Omog amempa mtihani mzito Emmanuel Okwi.

Image result for emmanuel okwi ngao ya jamii
KOCHA Mkuu wa Simba, Joseph Omog, amewapa mtihani washambuliaji wake wakiongozwa na Emmanuel Okwi na John Bocco baada ya kusema kuwa, msimu huu anataka kuona timu yake inafunga mabao mengi zaidi ya msimu uliopita ili isitokee wakakosa tena ubingwa kizembe.


Msimu uliopita, katika Ligi Kuu Bara, Simba ilifunga mabao 50 na kufungwa 17, huku Yanga ikifunga 57 na kufungwa 14, hali ambayo iliifanya Yanga kuwa bingwa kwa tofauti ya mabao 10 baada ya kumaliza msimu wote wakiwa na pointi 68.

Katika msimu huu, Omog anataka kuona Okwi na wenzake wanafunga mabao kuanzia 60 kwenda mbele kwani anaamini ndiyo yataweza kuwaweka katika nafasi nzuri ya kuwa mabingwa, huku safu yao ya ulinzi ikilinda vizuri wasiruhusu mabao mengi.
Mpaka sasa katika ligi kuu, Simba imeshafunga mabao saba ambayo manne yamefungwa na Okwi, huku Shiza Kichuya, Juma Liuzio na Erasto Nyoni kila mmoja akifunga bao moja.

“Tumeanza vizuri kwa kufunga mabao saba, dhamira yetu kubwa ni kuona tunafunga mabao mengi zaidi ya yale ya msimu uliopita ambayo hayakutosha kutufanya kuwa mabingwa na matokeo yake tukaukosa kwa tofauti ya mabao.

“Katika kufunga mabao mengi, ni lazima na sisi tujilinde sana ili tusiruhusu wapinzani wakatufunga sana kwani haitakuwa na maana nyie mkafunga mabao mengi, halafu pia mkafungwa mengi.

“Vile ambavyo Yanga walifanya msimu uliopita, ndiyo tunataka tufanye sisi msimu huu, kwa jinsi tulivyoanza nadhani ni mwanzo mzuri, tukiendelea hivi sidhani kama kuna timu itatuzidi kwa mabao, angalau washambuliaji akiwemo Okwi na wenzake wafunge kuanza mabao 60 na kuendelea,” alisema Omog.


No comments:

Post a Comment