Kufuatia bomoabomoa inayoendelea katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, wananchi wameunda kamati ya mazungumzo ili kuiomba serikali isitishe zoezi hilo kwani wamekuwa wakipoteza makazi yao.
Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda leo Agosti 30, ametembelea maeneo ya Tuangoma, Mbagala na kufanya mazungumzo na wananchi pamoja na waathirika wa bomoabomoa hiyo.
Aidha wananchi wa Tuangoma wametoa kilio chao kwa Makonda kuhusu migogoro ya ardhi iliyopo eneo hilo ambapo Mkuu huyo ameahidi kuishughulikia ipasavyo kwa kuwataka watendaji wa Wizara ya Ardhi na Mkuu wa Wilaya ya wahakikishe wanatatua migogoro hiyo mapema huku akimuagiza kuwakama wote waliotapeli ardhi ili wafikishwe kwenye mkono wa sheria.
Makonda amewataka wananchi kutonunua viwanja kwa kuidhinishiwa na wenyeviti wa mitaa kwani hawana mamlaka kisheria ya kuuza viwanja hivyo wamekuwa vyanzo vya migoro ya ardhi na bomoabomoa kwenye maeneo hayo.
Makonda pia amewasisitiza wananchi kushirikiana na polisi katika kupambana na uhalifu. Aliwakumbusha wananchi kuwa, mitandao haina nguvu ya kuwalinda dhidi ya uhalifu bali nafasi hiyo wapewe polisi kwani wamesomea mambo hayo huku akuwaonya waache kutoa majibu ambayo yanapotosha yale yanayofanywa na vyombo vya usalama. Amesisitiza kuwa, mitandao ya kijamii inatia hofu na kuwafanya wahalifu wakimbie.
No comments:
Post a Comment