Tuesday, 1 August 2017

Ripoti ya CHADEMA kuhusu Serikali ya Rais Magufuli.

Image result for Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Serikali imeshindwa kusimamia mfumuko wa bei ya chakula nchini kwa sababu haitambui umuhimu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).

Mbowe amesema mwakà 2015, NFRA ilihifadhi tani 446,000 za chakula lakini kufikia mwaka huu wakala huyo amehifadhi tani 74,826 za chakula.

Mbowe amesema chakula kinapanda bei kwa sababu hakuna mkakati wowote wa Serikali kuwainua wakulima kwa kuwapatia pembejeo za kilimo.

"Usalama wa taifa ni usalama wa chakula, kama hakuna usalama wa chakula hakuna usalama wa Taifa.

"Mtakubaliana na mimi kuwa kwa miaka hii miwili vitu vimepanda bei lakini kipato cha wananchi hakijaongezeka

"Bei ya mahindi kwa mwakà 2015 ilikuwa ndogo lakini mwaka huu imefika zaidi ya 90,000. Wananchi wanapata shida kwa sababu Serikali yao imewatupa wakulima." Amesema Mbowe

No comments:

Post a Comment