Thursday, 31 August 2017

Serikali yataifisha Magari yaliingizwa kinyume cha sheria.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetaifisha jumla ya magari sita yakiwepo magari matatu aina ya Ranger Rover Sports yaliyoingizwa nchini kinyume na sheria baada ya watuhumiwa hao kukiri kuwa wamefanya kosa hilo.


Rais Magufuli mwezi Machi mwaka huu alipokwenda bandarini alikuta kuna makontena yenye magari ndani yake huku wamiliki wa makontena hayo wakidai  makontena hayo yalikuwa na nguo na mabegi  lakini baada ya kufunguliwa zilionekana gari za kifahari zikiwa kwenye makontena hayo, jambo ambalo lilionekana wamiliki wa mahari hayo walikuwa wakiingiza magari hayo kinyume na utaratibu na sheria za nchi. 

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, DPP Biswalo Mganga amesema kuwa baada ya mahakama kuwakuta na hatia raia hao wakigeni ambao walidai kuwa kontena hizo zilikuwa na nguo na mabegi wakati ni magari hivyo serikali imetaifisha magari yao na sasa kuwa magari ya serikali.

"Rais hao wamekiri makosa yao yote mawili na kutokana na kukiri kwao mahakama imewatia hatiani na ikaamuru yale magari yote matatu kuyataifisha kuwa mali ya serikali na kila mmoja anatakiwa kulipa faini ya milioni 133 kufidia hasara ambayo serikali imepoteza na kila mmoja anatakiwa kulipa tena milioni tano kama faini ambayo mahakama imewalipisha , wakishindwa kulipa faini hiyo watakwenda jela miaka mitatu" alisema Biswalo.

Aidha Biswalo amesema kuwa magari yote sita ambayo Rais Magufuli aliyakuta bandarini yametaifishwa na kuwa mali ya serikali.

Mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu Rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza bandarini na kukuta kuna makontena ambayo wamiliki wake walidai ni makontena ya nguo na mabegi na nyaraka zilionyesha hivyo lakini yalipofunguliwa zilikuwa ni gari za kifahari, hivyo watu hao walikuwa wakikwepa kulipa kodi na kuitia hasara serikali.

No comments:

Post a Comment